Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema nahodha wa timu hiyo John Bocco anaendelea na program maalum ya mazoezi kabla ya kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza
Bocco ambaye yuko nje kwa miezi miwili, anatarajiwa kujumuishwa kikosini baada ya wiki moja
"Anaendelea na mazoezi mepesi na anaweza kujiunga na wachezaji wenzake kwenye mazoezi labda baada ya wiki moja na sio chini ya hapo," amesema Aussems
Akizungumzia maendeleo ya kikosi chake, Aussems amesema baada ya mapumziko ya michuano ya Kimataifa, wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo yote ya ligi itakayofuata
"Tutakuwa na michezo mitano katika kipindi cha siku 17. Tutaendelea kuwapa nafasi wachezaji tofauti tofauti ili kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michezo hiyo"
ADVERTISE HERE