Kwa hakika msimu huu kuna jambo kubwa litafanywa na Simba, mabingwa wa soka Tanzania Bara
Tangu wapotezea mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Sevilla mwishoni mwa msimu uliopita, Simba haijapoteza mchezo wowote
Msimu huu Simba imeshuka dimbani mara 15 katika mechi za kimashindano na zile za kirafiki
Mabingwa hao wa nchi wamepata ushindi katika mechi 10 na kulazimishwa sare katika michezo mitano
Simba wamepania msimu huu, kwanza wanataka kushinda mataji yote ambayo timu hiyo inashiriki bila ya kujali ukubwa wake
Lakini pia kuweka rekodi ya kutopoteza mchezo, wakipania kusahihisha makosa ya misimu miwili iliyopita
Mpaka sasa kikosi cha Patrick Aussems kinaonekana kuwa na uwezo wa kutimiza malengo hayo
Usajili makini uliofanywa umempa uhuru Aussems ambaye amesema ukubwa wa kikosi chake umempa matumaini ya kufanya vizuri msimu huu