Tairone, Fraga washangaza mashabiki Kigoma

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Oct 2019
Tairone, Fraga washangaza mashabiki Kigoma

Pamoja na Uwanja wa Lake Tanganyika kutotofautiana sana na viwanja vingi vya mchangani kutokana na ubovu wake katika eneo la kuchezea kutokuwa na nyasi, nyota wa Simba raia wa Brazil Tairone Da Silva na Fraga wameonyesha kumudu mazingira hayo

Katika mechi za kirafiki ambazo Simba imecheza mkoani Kigoma, Fraga akiwa katika dimba la kati, kama kawaida yake alikuwa akikata 'umeme' huku uchezaji wake ukionekana kutotofautiana na baadhi ya wachezaji wa Kitanzania ambao wamezoea viwanja vibovu.

"Huyu Fraga utafikiri Mbongo, sikutarajia kuona akimudu kucheza vizuri katika uwanja mbovu kama huu hasa ukizingatia ametoka Brazil ambapo tunaamini ni moja ya nchi yenye viwanja bora vya soka duniani," alinukuliwa Hamad Miraji na gazeti la Nipashe, shabiki huyo alishuhudia mechi kati ya Simba na Aigle Noir ya Burundi.

Shabiki mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Karim Ramadhan, alihoji:

"Hivi huyu Tairone na mwenzake Fraga kweli wametoka Brazil? Siamini macho yangu, kumbe hata mchangani wanaweza kuibeba timu! Kweli kama unajua, unajua tu."

Katika mechi ya kirafiki dhidi ya Bandari FC ya Kenya, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ben Mwalala, alimmwagia sifa Fraga kutokana na uwezo wake wa kutibua mipango ya mashambulizi, kukaba na kutoa pasi za haraka bila kupoteza muda hali iliyowapa wachezaji wake wakati mgumu wa kujipanga.

Tairone alionyesha uwezo wakicheza na Wawa kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar ambazo Simba walishinda mabao 3-0 kisha dhidi ya Biashara United mabao 2-0 na wakacheza kwenye mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Bandari ambayo walishinda kwa bao 1-0 kabla ya kuonyesha uwezo tena wakati wakitoka sare tasa dhidi ya Aigle Noir ya Burundi mkoani Kigoma.

Aussems alisema mabeki hao wamekuwa wakifanya vizuri na wanaelewana kwa sasa tofauti na zamani ndiyo maana wameweza kucheza kwa muda huo bila ya kuruhusu bao lolote la kufungwa.

“Hadi sasa hatujafungwa bao kwenye mechi ambazo Wawa amecheza na Tairone, jambo zuri ni kwamba wanaendelea kucheza kwa kuelewana kwa kadiri siku zinavyokwenda, lakini hilo haliwezi kuwa sababu yao kucheza kila mechi, hapa tuna wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza nafasi hiyo," alisema.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
13h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
14h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
16h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’