Mechi za kirafiki zinatuimarisha - Shamte

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Oct 2019
Mechi za kirafiki zinatuimarisha - Shamte

Beki wa Simba, Haruna Shamte amesema mechi za kirafiki zitawaweka katika mazingira mazuri ya kufanya vyema kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ligi Kuu imesimama wiki mbili kuipisha Taifa Stars inayojiandaa kucheza na Sudan katika mchezo wa kufuzu Fainali za Chan Ijumaa wiki hii.

Simba imecheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Bandari (ilishinda bao 1-0), Mashujaa (1-0), jambo ambalo Shamte analiamini linawajengea uwezo mzuri wa kushindana.

"Mechi za kirafiki ni nzuri zinakuwa zinaonyesha mapungufu yapo wapi na kumfanya kocha kurekebisha kikosi chake mapema na kukiandaa kilicho bora,"

"Pia ndani ya kikosi chetu kuna ushindani wa namba, hapo ndipo pakuonyesha jitihada zote ili kumshawishi kocha," alisema.

Alisema lengo kubwa ni kuendeleza ushindi ambao waliuanza ligi kuu na walishinda mechi nne.

"Ndio kuna wachezaji ambao wameitwa Stars, hivyo sisi tunatakiwa kuwa kwenye piki ili tukianza ligi tuendeleze ushindi ambao tulianza nao kwani huwezi kujua wapinzani wetu wanajipangaje," alisema.

Simba ilishinda mechi za ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar (2-1), Kagera Sugar (3-0), JKT Tanzania (3-1) na Biashara (2-0), hivyo kufikisha pointi 12 kwenye msimamo.

Leo itashuka dimbani mkoani Kigoma kuikabili Aigle Noir kwenye mchezo wa kirafiki

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
52m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’