Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib ni miongoni mwa wachezaji bora aliowahi uwafundisha hata hivyo amesema anahitaji muda zaidi ili kuweza kuwa fiti
Aussems ambaye yuko mkoani Kigoma na kikosi chake kwa ajili ya kucheza mechi mbili za kirafiki, amesema Ajib alikosa maandalizi mazuri ya mwanzoni mwa msimu kutokana na kuwa majeruhi hivyo ataendelea kuimarika kadiri anavyopata nafasi ya kucheza
Aidha, Aussems amesema kiwango kilichoonyeshwa na Ajib kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Bandari Fc ni ishara kuwa ameanza kuimarika
"Maswali napokea kuhusiana na kiwango cha Ajibu, labda niwaambie ni kati ya viungo bora wenye uwezo wa kuchezesha timu na kubadili matokeo ndani ya dakika 90," amesema
"Kikubwa Kilichosababisha ashindwe kuonyesha ubora wake ni majeraha yaliyomuwekea nje ya uwanja kwa muda mrefu na kusababisha kutokuwa na ‘pre season’ nzuri kwake"
"Na hiyo ilisababisha kukosa michezo miwili ya awali ya ligi, hivyo ninaamini kadiri atakavyokuwa anacheza mechi za ligi, basi atazidi kubadilika na kuonyesha kiwango kikubwa"
Ajib alifunga bao pekee la Simba kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Bandari Fc ambao ulipigwa mwishoni mwa wiki iliyopita uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam