Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Senzo Mazingiza atawasili mkoani Kigoma leo kuiunga mkono timu yake ambayo itacheza mechi mbili za kirafiki
Baadae Simba itashuka kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kumenyana na Mashujaa FC
Keshokutwa Jumatano itarejea tena dimbani hapo kuumana na Aigle Noir (Black Leopards)
Mazingiza amekuja na utaratibu tofauti ambapo amekuwa akisafiri na timu kila inapokwenda
Pamoja na kutimiza majukumu yake, Senzo amekuwa akitumia ziara hizo kutembelea Matawi ya klabu ya Simba mikoani huku akijipa muda wa kuifahamu vyema Tanzania
Senzo ni raia wa Afrika Kusini
ADVERTISE HERE