Mlinda lango namba mbili wa Simba Beno Kakolanya na kiungo Ibrahim Ajib jana walin'gara kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Bandari Fc, mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
Wakati Kakolanya akiokoa michomo ya hatari, Ajib alifunga bao pekee ambalo liliihakikishia Simba ushindi muhimu wa bao 1-0
Mwanzoni wapo waliokosoa ujio wa wachezaji hao Msimbazi lakini sasa hakuna mwenye mashaka
Beno na Ajib walin'gara wakati wakiwa Yanga, hakuna shaka wataendeleza moto huo Msimbazi

Ajib ameanza kuonyesha makali yake baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje mwanzoni mwa msimu
Beno amekuwa bora kila anapopewa nafasi, ataendelea kumpa changamoto Aishi Manula ambaye bado ndiye kipa namba moja wa Simba
ADVERTISE HERE