Mazingiza kuipeleka Simba 'Next Level'

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Oct 2019
Mazingiza kuipeleka Simba 'Next Level'

Kama kuna mpenzi yeyote wa Simba ambaye bado anaumizwa na kitendo cha timu yao kutolewa mapema katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hana haja ya kuendelea kuteseka kwani mambo mazuri yanakuja Msimbazi.

Mbali ya uwanja unaoelekea kukamilika eneo la Bunju, Dar es Salaam utakaoiwezesha Simba kutopoteza fedha kukodi viwanja vya kufanyia mazoezi, kuna mipango mingine madhubuti yatakayoifanya klabu hiyo kuwa tishio si tu Afrika Mashariki, bali pia Afrika kwa ujumla.

Kwa mikakati iliyopo katika faili la Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingiza, klabu hiyo ndani ya miezi michache ijayo, itaanza kuwa tishio ndani hadi nje ya uwanja, yaani kisoka na kiuchumi.

Bosi huyo raia wa Afrika Kusini, kazi yake ya kwanza ni kuhakikisha wanakuwa na kikosi bora kitakachowafanya mashabiki kuwa na furaha muda wote kwa timu yao kufanya vizuri uwanjani.

Katika hilo, Mazingiza ameanza kupitia mchezaji mmoja mmoja wa Simba kubaini ni yupi anastahili kuendelea kuwapo Msimbazi kutokana na kiwango chake na wapi wanatakiwa kutupiwa virago.

Kwa mujibu wa kiongozi wa ngazi ya juu Simba, Mazingiza amekuwa akiumizwa kuona kuna wachezaji wanalipwa fedha nyingi, lakini wakiwa hawaheshimu kazi yao, hivyo kuchukua hatua kadhaa zitakazomfanya kila mmoja kukitolea jasho kile anacholipwa.

“Baada ya haya mambo yaliyotokea hivi karibuni juu ya utomvu wa nidhamu ya wachezaji, kwa sasa naona wameshaanza kumwelewa…huyu jamaa hataki utani, yupo makini sana na kazi yake,” alisema kiongozi huyo ambaye hakupenda jina lake kuwekwa wazi.

Alisema kuna uwezekano mkubwa kipindi cha dirisha dogo akahitaji wasajiliwe wachezaji wawili au watatu ili kukiongezea nguvu kikosi chao, tayari kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), hali itakayowahakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu wa 2020/2021.

“Ukiacha na suala la kutengeneza timu ya ushindi, pia anataka tuwe na mfumo rasmi wa kuiingizia klabu pesa (fedha), ikiwamo kutengeneza wachezaji na kuwauza ili klabu iwe na uchumi imara,” alisema mtoa habari wetu huyo.

Aliongeza: “Senzo ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wa soka hapa nchini, kwake ‘Simba kwanza, mchezaji au kiongozi baadaye’, ndio maana wababaishaji wengi ndani ya Simba, watamchukia sana tukutokana na misimamo yake ambayo kwa mtu anayeipenda kwa dhati Simba, lazima atakubaliana naye.

“Huwa anasema klabu inatumia fedha nyingi sana kwa ajili ya timu. Sasa haiwezekani fedha ziteketee bure halafu ghakuna lolote la maana linalofanyika. Anakuhakikishia kwa msimamo wa huyu bwana, Mo (Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji) atampenda sana.”

Juu ya mpango wake huo, Mazingiza ameliambia gazeti la BINGWA kuwa uongozi wake huwa na mafanikio makubwa na kwamba hajawahi kuboronga katika sehemu zote alizopita.

 “Nimeona kasoro kadhaa ndani ya timu na hata kiuendeshaji ambazo zinahitaji mtu mwenye weledi zaidi. Binafsi nina uwezo wa kusaidia katika hilo. Huwa napenda kufanya kazi yangu kwa kuzingitia mikataba. Niwahakikishie mashabiki wa Simba sitawaangusha,” alisema.

Juu ya kikosi hicho, alisema: “Ninaingalia Simba kama klabu ambayo inastahili kuwa na mafanikio makubwa, kama Mungu akinisaidia kuwapo hapa zaidi ya miaka miwili, basi itakuwa klabu kubwa zaidi ya Arlando Pirates na nyinginezo Afrika.” 

Mazingiza alitua Simba mwezi uliopita akichukua mikoba ya aliyekuwa Ofisa Mtandaji Mkuu wa klabu hiyo, Crescentius Magori.

Bingwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’