Viwanja vya Mkwakwani, Namfua, Jamhuri vyafungiwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Oct 2019
Viwanja vya Mkwakwani, Namfua, Jamhuri vyafungiwa

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya saa 72) imezuia baadhi ya viwanja kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutokana na kuwa na upungufu katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la kuchezea (pitch) na uzio wa ndani unaotenganisha wachezaji na washabiki (fence).

Viwanja hivyo ni Kinesi Bull (Dar es Salaam), Bandari (Dar es Salaam), Jamhuri (Morogoro), Namfua (Singida), na Mkwakwani (Tanga). .

Klabu ambazo timu zao zinatumia viwanja hivyo zimepewa nafasi ya kufanya marekebisho kipindi hiki ambacho Ligi zimepisha mechi za kirafiki za FIFA au kuchagua viwanja mbadala vyenye sifa.

Vilevile klabu zimekumbushwa kuwa kwa mujibu wa kanuni, zinapaswa kupeleka viwanjani gari ya wagonjwa badala ya gari yenye kitanda kwani kanuni ya 14(2) imetaja ambulance na si gari lolote.

"Wasimamizi wa mechi vituoni wanatakiwa kuhakikisha ambulance zinapokuwepo viwanjani kama ilivyoelekezwa kikanuni. Kama huduma ya ambulance haitokuwepo wanatakiwa kuzuia mechi kuchezwa", imeeleza taarifa iliyotolewa na kamati hiyo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’