TFF yamuonya Mauya kwa kumshambulia Ajib

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Oct 2019
TFF yamuonya Mauya kwa kumshambulia Ajib

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya saa 72) imempa onyo kali mchezaji Zawadi Mauya wa Kagera Sugar kwa kosa la kumpiga mateke mchezaji wa Simba Ibrahim Ajibu kwenye mechi iliyochezwa Septemba 26, 2019 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Taarifa iliyotolewa leo na TFF imeeleza kuwa kamati hiyo pia imempa onyo mwamuzi wa mchezo huo Emmanuel Mwandembwa kwa kumuonesha Mauya kadi ya njano badala ya nyekundu kwa kitendo hicho ambacho kilikuwa cha makusudi na kujirudia.

Adhabu nyingine zilizotolewa na kamati hiyo ni kama ifuatavyo.

Lipuli FC 2-2 Tanzania Prisons: Klabu ya Tanzania Prisons imetozwa faini ya shilingi 3,000,000 (milioni tatu) kutokana na basi lililobeba wachezaji wa timu hiyo kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi hiyo iliyofanyika Septemba 29, 2019 kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Coastal Union 2-0 KMC: Klabu ya KMC imetozwa faini ya shilingi 1,000,000 (milioni moja) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa Septemba 13, 2019 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Alliance FC 1-1 Biashara United: Klabu ya Alliance imetozwa faini ya jumla ya shilingi 1,000,000 (milioni moja) kutokana na vurugu za mashabiki wake pamoja na kufanya vitendo vinavyoashiria imani za ushirikina katika mechi hiyo iliyofanyika Septemba 20, 2019 kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Nayo klabu ya Biashara United imetozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kufanya vitendo vinavyoashiria imani ya ushirikiana wakati ikiingia uwanjani.

Singida United 0-1 Alliance FC: Klabu ya Alliance imetozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kumuweka kwenye benchi la ufundi meneja ambaye hakutambulishwa katika kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) wakati wa mechi hiyo iliyofanyika Septemba 28, 2019 kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’