Leo Ijumaa Oktoba 11 2019 umetimia mwaka mmoja tangu tukio la kutekwa Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' liitikise nchi
Mo amesema tukio hilo hatalisahau kamwe kwani katika kipindi chote alichokuwa akishikiliwa, aliishi bila ya kuwa na uhakika wa kuiona kesho yake
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Mo ameandika ujumbe huu;
"Mwaka mmoja uliopita siku kama ya leo nilitekwa. Siku 9 nilizofungwa macho na mikono kilikuwa ni kitendo cha mateso zaidi kwenye maisha yangu yote"
"Kutokuwa na uhakika wa kuona dakika inayofata nikiwa hai ilikua ni hali ya kutisha, lakini nashukuru Mwenyezi Mungu, na sala za wengi, nilivuka shida zote"
"Kurudi kwangu salama ndio ushuhuda wa kweli wa nguvu ya maombi"
"Nilibarikiwa kwa kupewa nafasi ya pili ya maisha. Asanteni Watanzania wenzangu wote na kila mtu duniani kote kwa maombi yenu na msaada usio na shaka"
"Mwenyezi Mtukufu awasimamie katika mambo yenu kwa upendeleo mkubwa! Ameen"
