Aussems kubadilisha kikosi mechi dhidi ya Bandari Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Oct 2019
Aussems kubadilisha kikosi mechi dhidi ya Bandari Fc

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema michezo mitatu ya kirafiki wanayotarajia kucheza, ataitumua kuwapa nafasi wachezaji ambao wamekosa muda wa kutosha kwenye kikosi cha kwanza

Aussems ambaye kikosi chake Jumamosi kitashuka uwanja wa Taifa kuikabili Bandari Fc, amesema mchezo huo ni sehemu ya mazoezi kwa vijana wake

"Tunawakosa wachezaji saba ambao wako timu za Taifa hivyo sio mchezo ambao tunaweza kuutumia kujiimarisha kimbinu," amesema

"Ni mchezo wa mazoezi ambao nitautumia kuwapa wachezaji wengine nafasi ya kucheza"

Simba imeendelea kujifua uwanja wa Gymkhana hata hivyo mazoezi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara yamekuwa yakiathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam

Aussems amesema hilo linaweza kuwaathiri vijana wake Jumamosi kwani wamekosa muendelezo wa program za mazoezi kutokana na mvua hizo

Baada ya mchezo huo Simba itaelekea mkoani Kigoma, Oktoba 14 ikitarajiwa kucheza na Mashujaa Fc kisha kukamilisha ratiba yake kwa kucheza na Aigle Noir Oktoba 16 hukohuko Kigoma

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’