Nahodha wa Simba John Bocco ameanza mazoezi mepesi tayari kurejea kikosini baada ya kuwa nje kwa zaidi ya wiki saba
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema mkongwe huyo amepona majeraha na ameanza mazoezi mepesi
"Bocco amerejea na ataonekana hivi karibuni akiwa na wenzake ikiwa ni baada ya kuwa nje kwa miezi kadhaa kutokana na kupata majeraha ambayo yamemfanya akose mechi zetu za ligi na michuano ya kimataifa," amesema
Kurejea kwa Bocco ni habari njema kwa kikosi cha Patrick Aussems kuelekea mchezo dhidi ya Azam Fc Oktoba 23
Bocco aliumia kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam August 17, anaweza kuwa fit kuwavaa waajiri wake hao wa zamani
ADVERTISE HERE