Simba kuhamia Bunju mwisho wa mwezi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Oct 2019
Simba kuhamia Bunju mwisho wa mwezi

Meneja wa klabu ya Simba Patrick Rweyemamu amesema kikosi cha timu hiyo kitaanza kufanya mazoezi katika viwanja vyake Bunju mwishoni mwa mwezi huu

Rweyemamu amesema matengenezo ya viwanja hivyo yako katika hatua za mwisho ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa Novemba kila kitu kitakuwa tayari

"Tunategemea kuanza kuvitumia viwanja vyetu mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa Novemba," amesema

"Tuna faida moja, Bunju tutakuwa na viwanja viwili kimoja cha nyasi asili na kingine cha nyasi bandia hiyo itatupunguzia usumbufu na gharama za viwanja vya mazoezi"

"Tunawashukuru wote waliosimamia mchakato huu tangu kupatikana kwa eneo mpaka mwekezaji kukamilisha ujenzi. Ilikuwa ni ndoto ya kila Mwanasimba kuona jambo hili linafanikiwa"

Wakati huohuo Simba imeendelea na mazoezi leo kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Bandari Fc ambao utapigwa Jumamosi, Oktoba 12 kwenye uwanja wa Taifa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’