Kwasi kuikosa Ndanda FC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Dec 2017
Kwasi kuikosa Ndanda FC
Beki mpya wa Simba, Asante Kwasi raia wa Ghana ameondolewa kwenye kikosi kitakachoivaa Ndanda FC ambayo ni mechi ya Ligi Kuu mzunguko wa 12 kwa kuwa hajafanya mazoezi ya pamoja na wenzake kutokana na kuchelewa kukamilika kwa usajili wake.

Usajili wa Kwasi ulikuwa na utata baada ya Simba kufanya mazungumzo na kumpa mkataba mchezaji huyo wakati bado ana mkataba na timu yake japokuwa baadaye walikaa mezani na kumalizana na klabu yake ya Lipuli FC.

Kwasi ambaye awali aliwekwa katika Hoteli ya Spice iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam juzi Jumanne aliwasili akitokea Iringa alikokwenda kukusanya kila kilicho chake na kujiunga rasmi na kambi hiyo ambapo leo Jumatano asubuhi alianza mazoezi ya ufukweni ambayo ni maalumu kwa ajili ya kumuweka fiti kabla hajajiunga na mazoezi ya pamoja na wenzake.

Simba chini ya Kocha Masoud Djuma, iliendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Polisi, huku Kwasi akifanya mazoezi yake katika ufukwe wa Coco ambapo kocha Djuma amesema kuwa amemtengea mazoezi hayo maalumu na hatacheza mechi ijayo dhidi ya Ndanda FC.

Kwasi ataanza kuichezea Simba rasmi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi ambayo inatarajia kuanza hivi karibuni visiwani Unguja, Zanzibar.

"Ni mazoezi yake maalumu maana hajafanya mazoezi na wenzake hivyo ni lazima ajiweke fiti kwanza na mechi ijayo tutakayokwenda Mtwara yeye hatacheza, hayo mazoezi yatakuwa ya muda na atajiunga na wenzake," alisema Djuma

Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka kesho Alhamisi kuelekea Mtwara ambako watacheza mechi hiyo ya ligi na baadaye kwenda Zanzibar kwa ajili ya Kombe la Mapinduzi na ligi itasimama kwa muda.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17m ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
18h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’