Nahodha wa Simba Method Mwanjali amemwagia sifa mlinda lango namba moja wa timu hiyo Aishi Manula kuwa amekuwa msaada mkubwa tangu ajiunge na wekundu wa Msimbazi.
Mwanjali akizungumzia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stand United, Mwanjali amesema ushindi huo ulikuwa halali kwa Simba kwani timu ilicheza vizuri.
"Wachezaji wote tumepambana vyema dhidi ya Satand United, kuna makosa tulifanya katika safu ya ulinzi, lakini kipa Aishi Manula alitubeba na tunampongeza kwa uwezo wake mkubwa golini. Yeye ni msaada kwa timu yetu," amesema Mwanjali.
Simba iko kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kujikusanyia alama 11 sawa na Mtibwa Sugar na Azam FC.
Simba imefunga mabao mengi kuliko timu yoyote kwenye ligi kwani mpaka sasa imefunga mabao 14 na kufungwa matatu.

ADVERTISE HERE