Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Senzo Mazingiza umevunja ukimya juu ya sintofahamu ya taarifa iliyoibuliwa kwenye mitandao ya kijamii hapo jana
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya CEO mapema leo, imesema wachezaji Gadiel Michael, Clatous Chama, Erasto Nyoni na Jonas Mkude walifikishwa kwenye Kamati maalum ya Nidhamu kutokana na tuhuma zilizokuwa zikiwakabili
Wachezaji hao walifikishwa kwenye Kamati hiyo iliyokutana Oktoba 03 baada ya kukosa michezo miwili ya ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar na Biashara United
Taarifa hiyo imesema wachezaji hao wameruhusiwa kwenda kujiunga na timu za Taifa, uongozi utazungumza nao baada ya kurejea klabuni
Aidha, uongozi wa Simba umekanusha taarifa zinazodai kuwa wachezaji hao wamesimamishwa mwezi mmoja. Walisimamishwa kuhudhuria mazoezi wakati masuala yao yanajadiliwa na Kamati ya Nidhamu
Mtendaji Mkuu wa Simba Bw. Mazingiza ameahidi kutoa taarifa kwa Wanahabari juu ya hukumu iliyofikiwa kuhusu wachezaji hao
Katika hatua nyingine Simba imethibitisha kuwa kiungo wake Francis Kahata alipewa ruhusa kwenda kushughulikia masuala binafsi kwao Kenya
Kahata amerejea leo kuungana na timu