Simba vs Bandari Fc ni mechi ya kisasi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Oct 2019
Simba vs Bandari Fc ni mechi ya kisasi

Pamoja ya kuwa ni mchezo wa kirafiki, mechi kati ya Simba dhidi ya Bandari Fc itakayopigwa Jumamosi Oktoba 12 kwenye uwanja wa Taifa inatarajiwa kuwa na upinzani mkali

Mapema mwaka huu katika michuano ya Sportpesa Cup, Simba ilikutana na Bandari Fc hatua ya nusu fainali na kupoteza mchezo kwa kufungwa mabao 2-1

Simba ilitangulia kufunga bao lake kupitia kwa Meddie Kagere kabla ya Bandari kusawazisha na kufunga bao la pili

Bandari inashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika na inasubiri droo ya raundi ya mwisho kuelekea hatua ya makundi

Licha ya kuwakosa baadhi ya nyota wake walioitwa timu ya Taifa, kikosi cha Simba kiko imara na bila shaka kitawapa Burudani mashabiki wake Jumamosi

Wachezaji walioitwa timu ya Taifa ni Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Miraji Athumani

Kocha Patrick Aussems amesema mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Oktoba 23 kwenye uwanja wa Uhuru

Kutokana na umbali wa mchezo huo, Aussems ametaka vijana wake wapate mechi za kirafiki ambazo zitawaweka katika hali ya ushindani

Simba imeanza vyema msimu wa ligi kuu ikifanikiwa kushinda mechi zote nne za kwanza, imejikita kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 12

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’