Mkude nyota mwenye heshima Simba lakini..

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Oct 2019
Mkude nyota mwenye heshima Simba lakini..

Ukizungumzia wachezaji waliojijengea heshima kubwa kwenye klabu ya Simba, kiungo Jonas Mkude ni mmoja wapo

Mkude alijiunga na Simba mwaka 2010 akiwa kijana mdogo, na ameendelea kudunda Mitaa ya Msimbazi kwa miaka tisa sasa

Kwa sasa yeye ndio mchezaji aliyedumu Simba kuliko mwingine yeyote

Kazi yake uwanjani inaonekana na kuheshimiwa na mashabiki

Kama asingekuwa mchezaji mzuri, asingekuwa Simba kwa miaka yote hiyo

Lakini nje ya uwanja Mkude amekuwa akikabiliwa na changamoto za hapa na pale

Mara kadhaa ameingia kwenye mvutano na viongozi wa Simba na hata baadhi ya makocha akituhumiwa kuwa mtovu wa nidhamu

Amekuwa hana nafasi ya kudumu timu ya Taifa si kwa sababu sio mchezaji mzuri, makocha wamekuwa wakimuacha wakitoa sababu za aina hiyohiyo

Tukio la hivi karibuni ni mwendelezo wa matukio yanayomchafulia heshima yake

Sina shaka, uongozi wa Simba utatumia busara kumaliza sintofahamu iliyojitokeza.

Lakini umefika wakati Mkude inafaa ajitambue na kuheshimu thamani anayopewa Simba

Haileti picha nzuri kwa mchezaji mwandamizi kama yeye kuingia kwenye mgogoro na uongozi sababu ya masuala madogo

Pia kuwa na nidhamu ya kazi ni jambo ambalo litamnufaisha kwenye maisha yake ya soka

Kwani bado ana muda mrefu wa kucheza soka kutokana na umri wake

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’