Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems leo asubuhi alifuta program ya mazoezi ya kikosi chake kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam
Tangu jana Simba imekuwa ikitumia uwanja wa Uhuru kufanya mazoezi yake kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Bandari Fc ambayo itapigwa kwenye uwanja huo Jumamosi
Hata hivyo mvua iliyoanza kunyesha mapema leo imesababisha maji kufurika dimbani kupelekea benchi la ufundi kusitisha mazoezi
Simba inatarajiwa kucheza mechi tatu za kirafiki yakiwa ni maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Oktoba 23
ADVERTISE HERE