Hatma ya Mkude kufahamika baada ya Oktoba 18

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Oct 2019
Hatma ya Mkude kufahamika baada ya Oktoba 18

Uongozi wa klabu ya Simba utaweka wazi hatma ya kiungo wake Jonas Mkude ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya utovu wa Nidhamu

Suala la Mkude tayari limeshajadiliwa na Kamati ya Nidhamu ya klabu ya Simba ambapo mwenyewe alipewa nafasi ya kujitetea

Hata hivyo uongozi wa Simba umeona sio vyema kutoka hukumu wakati huu ambao kiungo huyo fundi anakabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa

"Suala la Mkude limesimama kwa muda kwa sababu ya kuitwa katika kikosi cha Stars, hukumu yake ilikuwa itolewe leo (jana) Jumatatu, lakini ameshajieleza na sisi viongozi wa timu, pia tulitoa taarifa kwa upande wetu, " alibainisha mmoja wa viongozi aliyekuwa kwenye Kamati iliyokuwa ikijadili suala hilo

Mkude anakabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa ambapo Oktoba 14 Stars itacheza na Rwanda ukiwa ni mchezo wa kirafiki ambao uko kwenye kalenda ya FIFA

Oktoba 18 Stars itarudiana na Sudan katika mchezo wa kusaka tiketi ya michuano ya CHAN kwa wachezaji wa ndani

Mchezo huo utapigwa nchini Uganda

Mkude alifikishwa kwenye kamati ya Nidhamu ya klabu ya Simba baada ya 'kukacha' safari kanda ya ziwa bila ya kutoa taarifa kwa uongozi wa timu hiyo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
34m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’