Kabla ya kuelekea mkoani Kigoma, kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Bandari Fc ya Kenya
Mchezo huo utapigwa uwanja wa Uhuru siku ya Jumamosi, Oktoba 12
Baadae Simba itaelekea Kigoma ambako Oktoba 14 itacheza na Mashujaa Fc mchezo ukipigwa uwanja wa Lake Tanganyika
Oktoba 16 Simba itarejea tena kwenye uwanja huo kuikabili Aigle Noir, mabingwa wa Burundi
Michezo hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Simba kuelekea mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Oktoba 23 kwenye uwanja wa Uhuru
ADVERTISE HERE