Djuma aipigia mahesabu Ndanda FC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
27 Dec 2017
Djuma aipigia mahesabu Ndanda FC
Wakati ikiwa tayari imeshapoteza nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao, klabu ya Simba sasa mbio zake ni kuhakikisha inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, ili kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Tiketi iliyobaki kwa klabu hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ili kuweza kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambayo huandaliwa na Shrikisho la Soka Afrika (Caf).

Hiyo ni kutokana na kutolewa kwenye Kombe la Shirikisho Tanzania na Green Warriors kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika timu hizo zikitoka sare ya bao 1-1.

Kutokana na kulitambua hilo, Simba ilichukua hatua kwa kumtimua Kocha Mkuu, Mcameroon Joseph Omog na timu hiyo sasa kubaki mikononi mwa Kocha Msaidizi, Masoud Djuma.

Na wakati huu mambo yakiwa bado hayajatulia, Djuma ameanza kuwapigia ‘mahesabu’ wapinzani wao, Ndanda FC watakaocheza nao Jumamosi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Djuma amekipeleka kikosi chake hicho kambini jana kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nangawanda Sijaona mjini Mtwara.

Djuma amesema wamelazimika kuanza mikakati mapema kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

“Timu inaingia kambini leo, hatutaki kufikiria kuhusu matokeo kwenye mchezo wetu uliopita wa Kome la Shirikisho, mawazo yetu tunaelekeza kwenye mchezo huu wa ligi,”alisema Djuma.

Alisema kikubwa kwao ni ushindi na kutokana na upinzani uliopo kwenye msimamo wa ligi wanafahamu kupoteza mchezo kutawapa nafasi wapinzani wao kukaa juu.

“Kuendelea kukaa kileleni ni lazima tujitoe na kupambana katika kila mchezo, kwa kipindi hiki cha wiki moja tunajipanga na kuelekeza nguvu zetu kwenye mchezo dhidi ya Ndanda,” alisema Djuma.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi sawa na Azam FC wanaoshika nafasi ya pili huku ikiwaacha wapinzani wao Yanga kwa tofauti ya pointi mbili
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →