Wakati kikosi cha Simba kikijiandaa kuelekea mkoani Kigoma kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc, mabingwa hao watetezi watawakosa wachezaji wao nane ambao wanakabiliwa na majukumu ya timu za Taifa
Nyota saba wameitwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambayo Oktoba 14 itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rwanda
Aidha Mshambuliaji kinara wa mabao Meddie Kagere nae ataelekea nchini Rwanda kujiunga na kikosi cha timu hiyo tayari kuwakabili kina Nyoni, Mkude na wengineo
Wachezaji saba wa Simba walioitwa timu ya Taifa ni Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Miraji Athumani
Simba inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki mkoani Kigoma dhidi ya Mashujaa Fc na Aigle Noir, mabingwa wa Burundi