Kiungo fundi wa Simba Ibrahim Ajib amesema sapoti ya mashabiki ndio inayowafanya wapambane kuhakikisha wanashinda kila mchezo
Baada ya Simba kutolewa hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, tukio hilo liliwaumiza sana wachezaji
Lakini uungwaji mkono mkubwa wanaopata kutoka kwa mashabiki, umewafanya warejee haraka kwenye ushindani na kufanikiwa kushinda michezo yote minne ya ligi kuu
Ajib amerejeshwa kwenye kikosi cha kwanza na kocha Patrick Aussems baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje mwanzoni mwa msimu
Amesema kwa mzuka walionao na ubora wa kikosi chao, msimu huu wamepania kufanya mambo makubwa
Pamoja na ushindani uliopo kutokana na kila timu kujiandaa vyema, Ajib amesema kwao kila mchezo utakuwa kama fainali
"Kila mechi kwetu ni muhimu na tunacheza kwa kuamini kwamba ushindani ni mkubwa ila bado tutaendelea kupambana," amesema
"Kazi bado ipo kutokana na ukweli kwamba michezo ipo mingi kushinda kwetu michezo ya mwanzo kunatuongezea hali ya kujiamini katika michezo inayofuata"