Mshambuliaji wa Simba Miraji Athumani atapokea kitita cha Tsh Milioni Moja pamoja na kin'gamuzi cha Azam TV baada ya kuibuka mchezaji bora wa mwezi Septemba
Miraji amesema mafanikio aliyopata yamechangiwa na wachezaji wenzake katika klabu ya Simba, hivyo wanastahili kupata sehemu ya zawadi aliyopata
"Mpira sichezi peke yangu uwanjani na kama si wachezaji wenzangu nisingeweza kuifungia Simba mabao, kusababisha bao wala kuwa na kiwango ambacho kwa sasa ninacho," amesema
Miraji amekuwa na mwanzo mzuri tangu arejee klabu ya Simba akitokea Lipuli Fc
Tayari amefunga mabao matatu pamoja na kutengeneza mabao mawili
Kiwango chake kimempa nafasi ya kuitwa timu ya Taifa ambayo Oktoba 14 itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda na baadae kuelekea Uganda kuikabili Sudan Oktoba 18