Ili kuhakikisha timu inaendelea kubaki katika ushindani, kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Smba kitaelekea mkoani Kigoma ambako kitacheza mechi mbili za kirafiki
Mchezo wa kwanza itakuwa dhidi ya Mashujaa Fc na utapigwa Oktoba 09
Baada ya mchezo huo Simba itaendelea kusalia mkoani Kigoma ambapo Oktoba 11 watacheza na Aigle Fc, mabingwa wa Burundi
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema michezo hiyo itawasaidia kuiweka timu katika hali ya ushindani wakati huu ambao ligi imesimama kupisha kalenda ya FIFA
Wachezaji ambao hawakuitwa timu za Taifa watahusika kwenye michezo hiyo
Michezo ya Ligi Kuu itaendelea Oktoba 23 kwa Simba kuikabili Azam Fc
ADVERTISE HERE