Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema analazimika kubadili program za mazoezi ya kikosi chake kwendana na kalenda za CAF na FIFA
Kusimama wa ligi mara kwa mara kupisha michuano ya Kimataifa imekuwa changamoto kwa kocha huyo Mbelgiji akihofia wachezaji wake kupoteza kasi waliyonayo
"Program za mazoezi zitabadilika kulingana na ratiba yetu," amesema
"Tuna mchezo baada ya siku 20, tunahitaji kuwa na program ambayo italinda viwango vya wachezaji wetu"
"Kwa sasa hatutafanya mazoezi magumu sana, pia tunaangalia uwezekano wa kupata michezo ya kirafiki"
Mabingwa hao watetezi wanaendelea na mazoezi leo baada ya mapumziko ya siku moja
Simba itashuka dimbani Octoba 23 kuikabili Azam Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru
Mabingwa hao watetezi wanaongoza ligi wakiwa wamejikusanyia alama 12 wakishinda mechi zote nne walizocheza