Kocha Mkuu wa timu ya Wanawake wa Simba Queens Mussa Mgosi amesema Ijumaa ya wiki hii ataweka hadharani kikosi cha timu hiyo
Simba Queens ambayo hivi karibuni ilikuwa ziarani nchini Ujerumani, imepania kutwaa ubingwa msimu huu
"Kuhusu wachezaji wa Simba Queens watakuwa wazi siku ya ijumaa pale uwanja wa Jkpack saa kumi kamili wakicheza mechi na vijana wa under 20 ya Jkpack," amesema
"Baada ya hapo ndio orodha ya wachezaji watakao ipigania Simba Queens kupata ubingwa msimu huu itakuwa imetoka
"Kwa sasa tunashukuru mungu wachezaji wa msimu uliopita tulibakisha 11 na kuongeza wachezaji wapya 14 na tuna jumla ya wachezaji 25"
ADVERTISE HERE