Kagere, Miraji wataliza sana watu msimu huu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Sep 2019
Kagere, Miraji wataliza sana watu msimu huu

Wakati alipoumia nahodha John Bocco kulikuwa na wasiwasi kidogo kuwa pengine safu ya ushambuliaji ya Simba ingeyumba

Bocco aliumia kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc na ameendelea kuwa nje akitibiwa

Hata hivyo ujio wa Miraji Athumani umeondoa hofu hiyo

Mabao yake matatu aliyofunga mpaka sasa yanadhihirisha kuwa anamudu kuifanya kazi ya Bocco

Kwa kiwango anachoendelea kuonyesha pengine kinaweza hata kikampa wakati mgumu Bocco atakaporejea kikosini

Meddie Kagere na Miraji mpaka sasa ndio washambuliaji bora wa ligi kuu hadi kufikia raundi hii ya tano

Wakati Kagere akifunga katika kila mchezo, Miraji ameweza kufunga kwenye michezo mitatu

Miraji pia amehusika kumtengenezea Kagere moja ya mabao yake

Wawili hao wamekuwa mwiba mpaka sasa, kwa Miraji anaweza kuwa mbadala sahihi wa Okwi

Bado ni mapema, lakini ni wazi kasi hii waliyoanza nayo itasumbua timu nyingi msimu huu

Pengine huu unaweza ukawa msimu ambao Simba itatoa mfungaji bora wa ligi kuu atakayefunga mabao zaidi ya 30

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
16h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
19h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’