Baada ya kumaliza ratiba ya Kanda ya ziwa, kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam leo kuendelea na maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya KMC
Simba imefanikiwa kuondoka na alama zote sita katika michezo yao miwili waliyocheza dhidi ya Kagera Sugar na Biashara United
Mabingwa hao wa nchi wamefunga mabao matano huku wakiwa hawajaruhusu kufungwa bao lolote
Msafara wa Simba umerejea jijini Mwanza ambako watakwea 'pipa' kurudi Dar es salaam

ADVERTISE HERE