Mabingwa wa Tanzania Bara Simba leo wako wilayani Musoma kuendelea kuwapa furaha mashabiki wao watakaivaa Biashara United
Simba imeanza msimu kwa kishindo ikifanikiwa kushinda michezo yote mitatu ya kwanza na kufanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi
Vijana wa Patrick Aussems waliwasili Musoma mapema jana na jioni kufanya mazoezi katika dimba la Karume
Simba inajivunia uwepo wa mshambuliaji wake Meddie Kagere ambaye mpaka sasa amefunga mabao matano, akifunga kwenye kila mchezo
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema timu iko katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo utakaopigwa saa kumi jioni
Ushindi kwenye mchezo huo utaifanya Simba iendelee kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha alama 12
ADVERTISE HERE