Aveva, Kaburu bado mambo magumu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Sep 2019
Aveva, Kaburu bado mambo magumu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema inahitaji muda wa kulipitia jalada ili iweze kutoa uamuzi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu'.

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) aliwasilisha maombi ya kutaka Mahakama hiyo isitishe usikilizwajwaji wa shauri hilo.

Septemba 20, DPP aliwasilisha ombi hilo kutokana kusudio la kukata rufaa iliyowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Katika rufaa hiyo DPP, anapinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaondolea Aveva na Kaburu mashtaka ya utakatishaji fedha na kuwapa masharti ya dhamana

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema ameshindwa kutoa uamuzi leo kwa kuwa hakujipa muda wa kutosha hivyo analipitia upya jarada la kesi hiyo ili aweze kutoa maamuzi.

"Kutokana na kubanwa na majukumu nahitaji muda wa kutosha nalipitia upya jarada la shauri hili ili niwezi kutoa maamuzi," alisema Simba.

Shauri hilo liliahirishwa hadi Oktoba 11 mwaka huu atakapokuja kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao walikuwa wakikabiliwaa na mashitaka tisa ambapo Septemba 19 mahakama hiyo iliwaondolea mashtaka mawili ya utakatishaji fedha kwakuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuyathibitisha.

Mahakama ilitoa masharti ya dhamana kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili kila watakaosaini dhamana ya Sh 30 milioni kila mmoja.

Hata hivyo, mahakama hiyo iliawakuta na kesi ya kujibu katika mashtaka saba ambayo ni kughushi, kula njama, matumizi mabaya ya madaraka, kutoa nyaraka za uongo, na kutoa maelezo ya uongo ambayo upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’