Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar jana ni salamu kwa wale ambao wamekuwa wakizungumza zaidi
Aussems amesema kabla ya mchezo huo, wapinzani wao walikuwa wakizungumza sana, wao wamewajibu uwanjani
"Nafahamu wapinzani wetu walikuwa wakizungumza sana kabla ya mchezo lakini sisi hatukuwajibu tukisubiri siku hii ya leo (jana)," alisema Aussems
"Majibu mmeyaona... Nawapongeza wachezaji wangu, wamecheza vizuri na kufuata maelekezo tuliyowapa"
"Sasa tunaelekea Mara ambapo Jumapili tutakuwa na mchezo mwingine"
Mabingwa hao watetezi wanaongoza ligi wakiishusha Kagera Sugar kutokana na wingi wao wa mabao licha ya timu zote kuwa na alama tisa
Jumapili Septemba 29 Simba itacheza na Biashara United katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Karume wilayani Musoma