Meddie Kagere ameanza kwa kishindo ligi kuu ya Vodacom msimu huu akifunga katika kila mchezo ambao Simba imecheza mpaka sasa
Kagere amefikisha mabao matano aliyoyafunga katika mechi tatu
Katika mchezo wa kwanza dhidi ya JKT Tanzania Kagere alifunga mabao mawili, akawafunga Mtibwa Sugar bao moja kabla ya leo kuwaadhibu Kagera Sugar kwa kuweka kambani mabao mawili
Msimu uliopita aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu akifunga mabao 23
Dalili zimeanza kuonekana kuwa msimu huu anaweza kufunga zaidi ya mabao aliyofunga msimu uliopita
Kwani moto alioanza nao hakuonekani kuwepo mwenye uwezo wa kuuzima
ADVERTISE HERE