Mwanjali aisifu Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
26 Dec 2017
Mwanjali aisifu Simba
Pamoja na kuachwa katika kikosi cha Simba hivi karibuni, aliyekuwa beki wa timu hiyo, Mzimbabwe, Method Mwanjali, ameisifia klabu hiyo kwa kusema kuwa hajaona kama hiyo katika timu za Afrika alizocheza, kwani ni ya kipekee, huku akiitakia mafanikio mema kwenye michuano yake.

Beki huyu alikuwa nahodha wa kikosi hicho, ameachwa na Simba kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo huku nafasi yake ikichukuliwa na beki Mghana, Asante Kwasi.

Mwanjali alisema kuwa, licha ya kupitia timu kadhaa huko nyuma, Simba ni moja kati ya timu ambazo aliyafurahia maisha alipokuwa akicheza kwa takriban miaka miwili.

“Sina la kusema lakini najua Simba ni klabu kubwa na ya kipekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na jinsi ambavyo imekuwa ikipambana kuhakikisha inaweka historia katika ramani ya soka pamoja na inavyowatunza wachezaji wake.

“Kila la kheri na mafanikio mema katika michuano yote ambayo ipo mbele yao, wapambane na kuweza kufika mbali zaidi ya walipo sasa,” alisema Mwanjale.

Ikumbukwe kuwa, Mwanjale kwa muda ambao amecheza Simba, amefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la FA pekee msimu uliopita.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
12h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
14h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
15h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
17h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →