Mchezaji wa zamani wa timu ya Simba SC, na timu ya Taifa, mzazi wa mchezaji wa Ruvu Shooting Said Dilunga, mzee Abasi Dilunga, amefariki ghafla usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake, Chanika, Dar Es salaam, ulipo msiba.
Abasi Dilunga, enzi zake akicheza timu ya Taifa, aliwahi kuchaguliwa kuunda kikosi bora cha Afrika akiwa mchezaji pekee kutoka timu ya Taifa ya Tanzania, hii ni baada ya kucheza dakika chache akitokea benchi wakati timu yetu ya Taifa ikicheza na timu ya Taifa ya Nigeria, mjini Lagos.
Mazishi ya shujaa huyu, yatafanyika leo, saa 10.00 jioni, Kisarawe, mkoani Pwani
Marehemu ameacha wajane wanne na watoto 13
Innah Lillah Wainah Illah Rajiun
ADVERTISE HERE