Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema baada ya timu hiyo kupoteza michezo yote miwili dhidi ya Kagera Sugar msimu uliopita, wachezaji wana nafasi ya kudhihirisha ukubwa wa Simba msimu huu
Akizungumza leo baada ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo, Aussems amesema wanakwenda Kagera wakiwa na lengo la kuchukua alama zote tatu
"Yaliyotokea msimu uliopita ni hamasa kwa wachezaji kufanya vizuri kwenye mchezo ujao na nimeshawaambia inabidi tuwaonyeshe kwamba sisi ni Simba," amesema
"Tunaenda na malengo ya kuhakikisha tunashinda"
Msafara wa Simba unatarajiwa kuondoka kesho Jumatano tayari kwa mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Kaitaba siku ya Alhamisi, saa kumi jioni
ADVERTISE HERE