Kiungo Clatous Chama atakosa michezo ya Simba kanda ya ziwa baada ya kupata majeraha mazoezini
Kikosi cha Simba kitaondoka kesho asubuhi kuelekea Kagera kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar
Mchezo huo utapigwa Alhamisi, Septemba 26
Baadae timu itaelekea Mara ambako itachuana na Biashara United Septemba 29
Mkufunzi wa Simba Patrick Aussems amesema Chama pamoja na Gadiel Michael hawatajumuishwa katika safari hiyo wakiungana na nahodha John Bocco
ADVERTISE HERE