Aussems ataka mabao ya mapema Kagera

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Sep 2019
Aussems ataka mabao ya mapema Kagera

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems anaendelea kukiandaa kikosi chake tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar

Mchezo huo utapigwa keshokutwa Alhamisi kwenye uwanja wa Kaitaba

Katika mazoezi ya mabingwa hao wa nchi yanayofanyika uwanja wa Gymkhana, Aussems ameonekana kuwapa maelekezo wachezaji wake kuhakikisha wanapata mabao ya mapema

Msimu huu Aussems ameonekana kuweka mkazo katika kupatikana kwa mabao mapema

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya JKT Tanzania Simba ilifunga bao kwenye dakika ya pili huku mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ikifunga bao kwenye dakika ya 16

Mbelgiji huyo amesema ni muhimu kwa vijana wake kuhakikisha wanafunga bao ndani ya dakika ya 20 za kwanza ili kuweza kuwaweka wapinzani wao kwenye presha

"Unapofunga bao mapema linawaweka wapinzani wako kwenye presha hivyo kunakuwa na uwezekano wao kufanya makosa zaidi," alisema

"Tunafahamu Kagera Sugar ni timu nzuri, msimu uliopita walitufunga michezo yote miwili. Tutacheza kwa tahadhari lakini malengo yetu ni kushinda mchezo huo"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’