TFF yathibitisha, Kapombe atapata zawadi ya JPM kwa wachezaji wa Stars

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Sep 2019
TFF yathibitisha, Kapombe atapata zawadi ya JPM kwa wachezaji wa Stars

Beki wa Simba na Taifa Stars, Shomari Kapombe, sasa kimeeleweka baada ya kujumuishwa katika majina ya wachezaji yaliyopelekwa serikalini kwa lengo la kupatiwa viwanja vilivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli.

Rais Magufuli aliahidi kuwazawadia  wachezaji hao viwanja jijini Dodoma, baada ya kufanikiwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2019), zilizofanyika nchini Misri.

Kapombe hakuwa miongoni mwa wachezaji waliokwenda Ikulu, Dar es Salaam, kupongezwa na Rais Magufuli, baada ya kuifunga Uganda mabao 3-0 katika mchezo wa mwisho uliochezwa Machi 24, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa na kufuzu michuano hiyo.

Beki huyo alisahaulika katika zawadi ya Rais Magufuli kutokana na hakuwapo kwenye kikosi kilichocheza na Uganda, sababu alikuwa akiuguza jeraha aliloumia  Afrika Kusini ambako Taifa Stars iliweka kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho.

Kutokana na beki huyo kuumia akiwa katika majukumu ya Taifa, alishindwa kuitumika Taifa Stars michezo miwili ya kuwania kufuzu Afcon dhidi ya Lesotho na Uganda, hivyo kutojumuishwa na wachezaji wenzake waliokwenda kupongewa na rais.

Hata hivyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia Ofisa Habari na Mawasiliano,Clifford Ndimbo, amesema Kapombe ni miongoni mwa wachezaji watakaopata zawadi ya viwanja vilivyotolewa na Rais Magufuli na jina lake limepelekwa serikalini.

Ndimbo alisema TFF kupitia kamati ya mashindano iliona imjumujisha kwa sababu ni miongoni mwa wachezaji waliopigana hadi Stars kufuzu kushiriki Afcon 2019,  licha ya kukosa mchezo dhidi ya Uganda kutokana na kuuguza jeraha.

"Viwanja vilivyohaidiwa na Rais bado havijakabidhiwa kwa wachezaji kutokana na baadhi ya nyaraka kutokamilika.

"Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  aliitaka TFF kukamilisha nyaraka muhimu zinazoeleza mchango wa wachezaji katika kuifanikisha  Stars kwenda Misri ili zikabidhiwe ofisini kwake na kuanza mchakato wa kuwapatia viwanja vyema hati miliki ya majina ya wachezaji akiwamo Kapombe," alisema Ndimbo.

BINGWA

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’