Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Wallace Karia amesema beki Shomari Kapombe aliomba apumzishwe na majukumu ya timu ya Taifa ili aweze kupona majeraha yake
Baada ya Stars kupoteza mchezo dhidi ya Sudan kwa kufungwa bao 1-0, kumekuwa na mijadala mingi baadhi ya mashabiki wakihoji kutojumuishwa kwa beki huyo ambaye ni chaguo la kwanza kwenye klabu yake ya Simba
Karia amesema mchezaji huyo aliitwa lakini baadae mwenyewe aliomba aondolewe kwa kuwa bado hayuko 'fit' kwa asilimia 100
"Shomari Kapombe alimuomba mwenyewe Mwalimu wa timu ya Taifa ya kuwa bado hajapona vizuri, apumzike kucheza timu ya Taifa kwa muda. Bila shaka baadae ataweza kujumishwa kwenye timu kama Mwalimu atamuhitaji," amesema
Mwezi Juni Kapombe aliingia kwenye mvutano wa TFF baada ya kuondolewa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kilichokuwa kinaelekea Misri kushiriki michuano ya CHAN
TFF ilidai mchezaji huyo ni majeruhi huku Kapombe mwenyewe akisisitiza alikuwa vizuri isipokuwa aliomba apewe ruhusa ya kumalisha program ya mazoezi aliyokuwa amepewa na daktari wake kabla ya kuanza kufanya mazoezi na wengine