Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kinatarajiwa kuelekea mkoani Kagera kesho tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar
Mchezo huo utapigwa Alhamisi, Septemba 26 katika uwanja wa Kaitaba
Simba inakabiliwa na michezo miwili kanda ya ziwa. Baada ya kucheza na Kagera Sugar, Septemba 29 Simba itaelekea Mara kuikabili Biashara United
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuweza kupata matokeo kwenye michezo hiyo
Rweyemamu amesema ni mchezaji mmoja tu nahodha John Bocco ambaye hatajumuishwa kwenye safari ya kanda ya ziwa kwa kuwa ni majeruhi
Simba itakwenda Kagera kwa usafiri a Ndege
ADVERTISE HERE