Beki wa kushoto wa Simba Gadiel Michael hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo ambacho Alhamisi kitaikabili Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Gadiel alipata majeraha jana wakati akiitumikia Stars kwenye mchezo dhidi ya Sudan ambao ulimalizika kwa Stars kufungwa 1-0
Hata hivyo nahodha msaidizi Mohammed Hussin 'Zimbwe Jr' yuko fit na leo alishiriki mazoezi ya Simba uwanja wa Gymkhana
Gadiel na Zimbwe wameanza vyema majukumu yao msimu huu wakipokeza namba timu ya Taifa na Simba
ADVERTISE HERE