Beki Kennedy Juma bado hajaonja radha ya kucheza kikosi cha kwanza cha Simba kwenye michezo ya kimashindano
Beki huyo kisiki aliyesajiliwa kutoka klabu ya Singida United, amejikuta katika wakati mgumu wa kupata namba mbele ya Paschal Wawa, Erasto Nyoni na Tairone Da Silva ambao wanaonekana kuaminiwa na kocha Patrick Aussems
Kenney pamoja na Yusufu Mlipili wamekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Pamoja na kukiri kuwa hali hiyo inamuumiza, Kennedy amesema ataendelea kupambana ili amshawishi Aussems ampe nafasi
"Sikuja Simba kukaa benchi hivyo kutopata nafasi mara kwa mara ni jambo linaloniumiza sana. Lakini natambua hapa kuna wachezaji wenye uzoefu kuliko mimi hivyo napaswa kufanya kazi ya ziada kuweza kumshawishi Mwalimu," alisema
Kennedy alitua Simba kuchukua nafasi ya Paul Bukaba ambaye alitolewa kwa mkopo klabu ya Namungo Fc