Mhamasishaji namba moja wa Simba Haji Manara ambaye pia ndiye Afisa Habari na Msemaji wa klabu, ataendelea na majukumu yake kama zamani
Baada ya CEO mpya wa Simba Senzo Mazingiza kuanza majukumu yake, inaelezwa alipendekeza Manara aendelee kubaki na majukumu yake licha ya mchakato wa kupata Afisa Habari mpya kuwa tayari umefanyika
Mazingiza amembakisha Manara kwenye nafasi yake kutokana na kazi kubwa ambayo amekuwa akiifanya
Manara amekuwa rafiki wa mashabiki wa Simba, ni Mwanasimba anayefahamu vyema ni kitu gani mashabiki wanataka
Kurejeshwa kwake kumefuta rasmi mpango wa kuajiriwa Mwanahabari Gift Macha kuwa Afisa Habari wa Mabingwa hao wa Tanzania Bara
ADVERTISE HERE