Kiungo kiraka Gerson Fraga ameanza kujifunza lugha ya kiswahili
Fraga ni mchezaji anayependa kujifunza na inaelezwa ni mwepesi kushika mambo anayoelekezwa
Tayari raia huyo wa Brazil anaonekana kufurahia lugha ya kiswahili ambapo mwenyewe ameweka msisitizo wa kutaka kuifahamu haraka
Mwanzoni mwa msimu kocha Patrick Aussems alisema miongoni mwa mambo yaliyowachelewesha wachezaji hao kuingia kwenye mfumo wa Simba ni suala la lugha
Ukimuondoa Fraga ambaye anafahamu lugha ya kiingereza, Wilker Da Silva na Tayrone wao wanafahamu lugha ya kwao tu Brazil
ADVERTISE HERE