Tanzania imejiweka katika nafasi ngumu ya kukata tiketi ya michuano ya CHAN baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka Sudan katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
Licha ya kutawala mchezo kwa muda mwingi, timu ilikosa maelewano katika kushambulia hivyo kupoteza nafasi nyingi
Nafasi moja muhimu waliyoipata Sudan waliitumia kuandika bao la ushindi kupitia Yassir Mohammed baada ya kufanya shambulizi la kushitukiza
Ulikuwa ni mchezo uliochezwa kwa muda mwingi kwenye nusu ya goli la Sudan, Stars watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kupata mkatokeo
Sasa watalazimika kushinda kwa zaidi ya bao moja mchezo wa marudiano ambao utapigwa nchini Uganda Oktoba 18
ADVERTISE HERE