Mshambuliaji kinara wa mabao Meddie Kagere jana alishiriki mazoezi ya Gym ya kikosi cha Simba yakiwa ni maandalizi ya kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar
Inaelezwa katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Kagere alijitonesha majeraha aliyopata akiwa na timu ya Taifa
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems alisema baada ya uchunguzi walibaini kuwa majeraha yake hayakuwa makubwa hivyo walimpa mapumziko ili aweze kupona
Kuelekea mchezo huo utakaopigwa Alhamisi, Simba inawakosa baadhi ya nyota wake ambao ni majeruhi
Nahodha John Bocco bado yuko nje akiendelea na matibabu wakati Deo Kanda anaendelea na program maalum
Hata hivyo kurejea kwa Wilker Da Silva ni habari njema kwa kikosi cha mabingwa hao watetezi
Mchezo dhidi ya Kagera Sugar una umuhimu wa kipekee kwa Simba kuibuka na ushindi hasa ikizingatiwa msimu uliopita Kagera Sugar ilishinda mechi zote mbili dhidi ya Simba
Kagera ameanza vyema msimu akiwa ameshafunga mabao matatu, uwepo wake kwenye mchezo huo ni muhimu sana