Kocha msaidizi wa Simba Masudi Djuma, amewaambia wachezaji wa Simba kuwa anatarajia kufanya mambo matatu kwao na lazima wajipange.
Djuma alisema mambo aliyopanga kwa wachezaji hao ni kuwapa mifumo mitatu mipya ya uchezaji itakayotoa nafasi kwa wachezaji wote kucheza, lakini pia atakazia zaidia suala la nidhamu ili kuifanya Simba izidi kupaa.
Lakini kubwa alilosisitiza ni kwamba kuanza sasa wachezaji hao wajiandae kisaikolojia kwani amepanga kuvunja ustaa ndani ya timu.
Baadhi ya nyota wa Simba walithibitisha juu ya mambo hayo matatu ambayo kocha Djuma ameanza nayo fasta baada ya kupewa mikoba ya ikocha mkuu.<
Wachezaji hao walisema ni kweli Mrundi huyo tayari amewapa maelekezo hayo ambayo ataanza kuyafanyia kazi mara moja.
“Ametuambia kuwa kwa sasa ndani ya timu hakuna staa na kila mchezaji atacheza, ataanza na mifumo mitatu itakayotoa fursa kwa wote, huku akisisitiza nidhamu,†alisema mmoja wa wachezaji waandamizi wa Simba.
Kocha Djuma alisema anaanza kurudisha heshima ya klabu ya Simba na morali kwa mashabiki na wanachama kwa kuifunga Ndanda FC kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa mjini Mtwara.
“Nafahamu mashabiki na wanachama wamepoteza imani na timu yao, lakini nitahakikisha imani yao inarejea na hiyo ni kushinda mechi zijazo, tunachopaswa kukifanya sasa ni kusahau yaliyopita na kuangalia yaliyopo mbele yetu. Bado timu ni nzuri na kikosi ni kipana,â€.
Djuma alisema katika mazoezi ya jana Jumapili asubuhi alitumia muda wake kuzungumza na wachezaji ili kila mmoja kujua jukumu lake ndani ya timu.
“Nataka kila mmoja aelewe jukumu lake uwanjani, kwani tunachohitaji sasa ni ushindi pekee na si kitu kingine, hivyo Wana Simba wategemee baadhi ya mabadiliko yenye mafanikio katika timu,†alisema Djuma.
Djuma alisema mipango yake ni kurejesha Simba katika kiwango bora kwani anafahamu kiu ya Wanasimba wote ni mafanikio na kutwaa ubingwa wa VPL
“Kuhusu suala la nidhamu Simba ni jambo la ndani sana si kulitoa nje, ila binafsi napenda mchezaji afahamu majukumu yake mambo mengine. Nidhamu ni kitu cha msingi sana katika timu,†alisema Djuma.
“Omog alikuwa ni bosi wangu na nilimkuta ana mfumo wake japo wakati mwingine tulijadiliana, ila mimi nina mfumo wangu huo ambao mara nyingi napenda kuutumia, “alisema
Djuma ambaye amewataka mabosi wa Simba kumtafutia uwanja mwingine wa mazoezi kwani anasema ule wa Chuo cha Polisi, Kurasini sio mzuri kwa timu yake kujinoa hapo.

ADVERTISE HERE